Tembelea Child-Help International

×

Kuhusu CHT

Child Help Tanzania ni Shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa chini ya sheria ya taasisi zisizo za kiserikali, Na. 24 ya 2002. Usajili Na. 00NGO/R/0855 wa Disemba 2019.

Child-Help Tanzania ilianzishwa mwaka 2018, na iliteuliwa kuwakilisha shughuli za Kimataifa za kusaidia wa Watoto nchini Tanzania, kama vile usambazaji wa vifaa vya matibabu na upasuaji kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, mafunzo kwa watoa huduma za afya, uhamasishaji na utetezi, na utoaji wa Nyumba za Matumaini kwa ajili ya wazazi na watoto wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi. Child-Help Tanzania ilisajiliwa mwaka wa 2019 na kuwa moja ya vitengo vitano vya Child-Help International, vitengo vingine vikiwa ni Pamoja na Child-Help Belgium, Child-Help Italy, Child-Help Germany na Child-Help Netherlands.


Maono yetu

Kufikia 2050 watoto wote walio na Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi wanapaswa kuwa na mwanzo mzuri wa maisha yao.


Dhamira yetu

Kuwezesha kizazi ambacho, watoto walio na Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi wanakuwa watu wazima wanaostawi katika jamii jumuishi.


Maadili yetu

Msaada: Tunafanya juhudi za kutoa msaada wa kijamii na kiuchumi kwa waathiriwa wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi kupitia utetezi na uwezeshaji.

Uadilifu: Kuendelea kujituma kupitia dhamira yetu huku tukifikia viwango vya maadili na taaluma katika shughuli zetu zote za shirika kunahitaji heshima, uaminifu, uwazi, uwajibikaji na ushirikiano. Kwa kufanya hivyo, tunajenga uhusiano endelevu na washirika wetu na umma.

Mazingira jumuishi: Tunathamini mchango kutoka kwa watu wa tamaduni, makabila na asili tofauti za kijamii katika mazingira yetu ya kazi. Tunalinda umuhimu wa mazingira jumuishi na usawa ndani, katika mchakato wetu wa kuajiri, na nje, katika shughuli zetu. Tunafanikisha hili kwa kuunda mazingira ya kazi rafiki ambayo yanathamini mchango wa kila mmoja wetu, kwa kutumia tofauti zetu kuwa na ufanisi zaidi katika kufikia dhamira, na kwa kuheshimu na kujifunza kutokana na uzoefu wetu mbalimbali na njia za kufikiri.

Ushirikiano: Tunajitahidi kujenga mazingira ya mawasiliano na ushirikiano mzuri ili kufikia lengo moja. Tunafanya kazi pamoja kwa njia ambayo watendaji wanafahamu mwelekeo wa taasisi, majukumu yao, na jinsi ya kufikia malengo kwa pamoja.

 

Jifunze zaidi kuhusu Kazi Zetu

Nani ni Nani

Ifahamu timu ya CHT na bodi ya wakurugenzi

Tunafanya Nini

Jifunze zaidi kuhusu kazi zetu

Washirika

Jifunze zaidi kuhusu Washirika wetu

Habari

Habari zaidi
19.12.2023

Kufuata Houses of Hope

Msichana wa miaka 21, Rhune Bervoet, mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika upigaji picha katika Kask & Conservatory inayopatikana Ghent (Ubelgiji) atatumia mwezi mmoja katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, akiishi katika House of Hope. Katika ukurasa huu unaweza kufuata hadithi yake. Katika utangulizi, tulitaja zaidi kuhusu madhumuni ya blogu hii, na kile unachoweza kutarajia katika siku zijazo.
Katika Utangulizi tulizungumza zaidi kuhusu madhumuni ya blogu hii, na kile unachoweza kutarajia katika siku zijazo.

Soma zaidi
18.12.2023

Kontena kwenda Tanzania

Tulisafiri njia ndefu, kwa wakati na umbali, ili kupeleka vifaa kwa watoto wenye mgongo wazi na maji kwenye ubongo hadi mahali stahiki.

Soma zaidi

Lets Collaborate!

swSwahili