tembelea Child-Help International

×

Tunafanya Nini

Tunasaidia watoto na watu wazima wenye Mgongo wazi na Kichwa Kikubwa. Tunatoa huduma kama vile usambazaji wa vifaa vya matibabu na upasuaji kwa vituo vya huduma za afya, mafunzo ya watoa huduma za afya, uhamasishaji na utetezi, na utoaji wa Nyumba za Matumaini kwa wazazi na watoto wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi kwa ajili ya kuwajengea maisha bora ya baadae, mazingira endelevu na jumuishi kwa watoto wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi. Ili kufanikisha hili, Child-Help Tanzania inafanya kazi na wadau nchini Tanzania.

Kazi zetu

Matunzo Endelevu

Lengo na jukumu letu kuu ni kuwezesha na kuhakikisha watu wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi wanapata huduma muhimu kwa maisha yao na mustakabali endelevu. Huduma hizi ni pamoja na bima ya afya, Nyumba za Matumaini, mafunzo mbali mbali kama Udhibiti wa Haja Kubwa na Ndogo, elimu, na vifaa saidizi kama viti vya magurudumu, magongo, etc.

Usambazaji wa Vifaa vya Matibabu na Upasuaji .

Kama sehemu ya malengo yetu, tunatanguliza usambazaji wa vifaa vya matibabu na upasuaji kwa vituo shirikishi vya afya na vyama vya wazazi, na kuhakikisha upatikanaji rahisi wa vifaa hivyo. Muda mfupi baada ya kuzaliwa, mtoto lazima afanyiwe upasuaji ili kufunga mgongo au kuondoa maji kichwani. Kuchelewa kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara ya kudumu. Upatikanaji rahisi wa vifaa hivyo unaweza kuongeza uwezekano wa kuepuka madhara ya kudumu ya ki afya au hata kifo.

Mafunzo na Utetezi wa Sera

Timu yetu inashiriki kikamilifu katika kutetea watu wenye ulemavu na kuelimisha wanachama, washirika, na walengwa kuhusu masuala muhimu yanayo ambatana na malengo na dhamira yetu.

Uwezeshaji wa Kiuchumi

Ili kujenga mustakabali endelevu wa watoto, tunajitahidi kuwawezesha kiuchumi wazazi na vijana wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi kwa kuwekeza kwa wajasiriamali, au kutoa mafunzo kuhusu ujasiriamali na ujuzi kwa ajili ya soko la ajira.

swSwahili