Tembelea Child-Help International
Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) imeanza rasmi kutumia mbadala wa kisasa kwa kueka shunt kwa wagonjwa wa Hydrocephalus baada ya kupokea mashine ya ETV. ETV (Endoscopic Third Ventriculostomy) ni utaratibu maalum sana unaohusisha kupitia maeneo ya ubongo yaliyojaa maji ili kuunda njia, shimo la kutolea maji ya ziada yaliyokwama katika maeneo hayo.
Ikilinganishwa na shunt, hakuna miili ya kigeni inayowekwa, na makovu madogo zaidi. Hii inamaanisha kuna usumbufu mdogo, kiwango kidogo cha maambukizi, na muda mfupi zaidi wa kukaa hospitalini. Wataalamu wanasema kwamba kwa kuchagua wagonjwa ipasavyo, ujuzi wa anatomy ya upasuaji, na ufahamu wa matatizo yanayoweza kutokea, ETV ni utaratibu salama na unaofaa kutibu hydrocephalus ambao unakwepa matatizo ya muda mrefu yanayoweza kutokea na shunt.
Child Help International, pamoja na Child-Help Tanzania, walitoa mashine ya ETV kwa idara ya upasuaji wa neurolojia ya Dkt. Rabiel katika KCMC kama utekelezaji wa malengo ya shirika. Child-Help ina furaha kubwakuhusu maendeleo ya kiteknolojia na ina matumaini kwamba uwekezaji huu unaweza kuleta mustakabali bora wa huduma za afya.
Wakati wa mahojiano na kituo cha redio cha Moshi FM, Dkt. Rabiel alisema; “Kulingana na ripoti ya takwimu ya mwaka jana, tulifanya upasuaji kwa kesi karibu 150 za Hydrocephalus na Mgongo Wazi. Hii inaonyesha kuwa tatizo bado lipo na ni kubwa. KCMC ina eneo kubwa la utawala likiwemo Manyara, Arusha na Tanga…”