tembelea Child-Help International

×

Washirika

Jinsi tunavyowezesha Washirika wetu

Child help Tanzania huunda ushirikiano wa kimkakati na watoa huduma za afya pamoja na vyama vya Wazazi ili kufikia malengo yake ya msingi ambayo ni kuhakikisha wanawapa maisha bora watoto wenye Kichwa kikubwa na Mgongo Wazi nchini Tanzania. CHT pia ina malengo ya kutanua mbawa zake na kushirikiana na mashirika ambayo yanaweza kuchangia dhamira yake.

Baadhi ya mafanikio yetu kutokana na ushirikiano huu ni pamoja na:

  • Usambazaji ulioboreshwa wa vifaa vya matibabu na upasuaji kama vile Shunts, Catheters, Oxybutynin, Mashine za ETV, Mashine za Ultrasound na vifaa vya usafi kwa ajili ya hospitali na vituo vya afya.
  • Kusaidia ‘Nyumba za Matumaini’ zilizopo Mwanza, Zanzibar, Dar es Salaam na miradi mingine nchini Tanzania.
  • Kuratibu mafunzo na programu za kufundisha kama vile Udhibiti wa Haja Kubwa na Ndogo, usimamizi wa nyumba za Matumaini (HoH), mafunzo ya matibabu, nk.
  • Uhamasishaji na utetezi wa kichwa kikubwa na mgongo wazi kwa kushirikiana na vyama vya wazazi.
  • Harambee kwa ajili ya watoto wenye Kichwa Kikubwa na mMgongo Wazi.

 

Washirika wa Kitaifa (Watoa Huduma za Afya)

Dar es Salaam:

Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) Taasisi ya Tiba ya Muhimbili (MOI) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 7 ya mwaka 1996 ikiwa na lengo kuu la kutoa huduma bora, zenye usawa, na zenye gharana nafuu katika fani ya Tiba ya Mifupa, ubongo, mishipa ya fahamu, n.k. Zaidi ya hayo, MOI inatoa mafunzo ya utoaji huduma bora kwa jamii.

Mwanza:

Bugando Medical Centre (BMC) Kituo cha Tiba cha Bugando (BMC) ni hospitali ya rufaa katika Kanda ya Ziwa na Magharibi mwa Tanzania. Inapatikana kando kando ya Ziwa Victoria katika Jiji la Mwanza. Ni hospitali ya rufaa inayotoa huduma maalum na za kitaalam.

Moshi:

Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) ni mojawapo ya hospitali nne za Kanda nchini Tanzania. Ilianzishwa rasmi mnamo 1971 kama hospitali ya Rufaa ya Kanda. Ilianzishwa ili kuhudumia ukanda wa kaskazini, mashariki na kati ya Tanzania.

Manyara:

Haydom Lutheran Hospital  (HLH) .

Mbeya:

Lutheran Hospital  (HLH) .


 

Washirika wa Kitaifa (Vyama vy Wazazi)

Dar es Salaam:

Zanzibar:

 


 

Washirika wa Kimataifa (Vitengo vya Chid-Help International)

Child-Help Tanzania hutoa uelewa katika Ulimwengu wa Kaskazini juu ya hali ya watoto na watu wazima wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi nchini Tanzania. Child-Help Tanzania ni miongoni mwa vitengo vitano vya Child-Help International. Vitengo vingine ni Child-Help Belgium, Child-Help France, Child-Help Germany na Child-Help Netherlands. Vitongo hivi hujenga vituo vya afya vinnavyojihusisha na kutoa matunzo maalum kwa watoto na watu wazima wenye ugonjwa wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi katika mataifa ya kusini ikiwemo Tanzania.

swSwahili