Tembelea Child-Help International

×
Terug naar overzicht

Ushuhuda wa Matibabu ya Mapema.

Mama anashiriki ushuhuda wake jinsi matibabu ya mapema yalivyompa binti yake maisha ya afya na ya kawaida.
Esther Milimo anaishi Dar es Salaam na ni mama wa msichana aliyezaliwa na Hydrocephalus. Esther anashiriki hadithi yake ya jinsi matibabu ya mapema yalivyomsaidia binti yake kuishi maisha ya kawaida na yenye afya, bila matatizo.
Mtoto wangu aligunduliwa na Hydrocephalus. Kabla ya kugundua kwamba alikuwa na Hydrocephalus, niligundua kwamba Sehemu ya juu ya kichwa chake inahisi laini, na haina mapigo ya moyo. Mara tu nilipoona ishara hizi, nilienda kwa daktari. Nilielekezwa kwa Hospitali ya MOI ambapo binti yangu alifanyiwa upasuaji wa kuweka shunt kwa mafanikio akiwa na umri wa miezi mmoja tu. Leo, anastawi vizuri. Huwezi hata kutambua kuwa aliwahi kuwa na tatizo hilo unapomwona. Namshukuru timu ya MOI kwa huduma yao na ningependa kuwahimiza wazazi waangalie watoto wao mapema kwa dalili yoyote ya wasiwasi. Ugunduzi wa mapema na matibabu yanaweza kuzuia matatizo ya muda mrefu na ulemavu.” Anasema Esther
CHT inafanya kazi kwa karibu na idara ya Neuro-surgery katika Hospitali ya MOI na hutoa shunti kwa kesi za Hydrocephalus. CHT pia inahamasisha matibabu ya mapema na inawahimiza wazazi kuharakisha watoto wao kwenda hospitalini kwa matibabu. Matibabu ya kuchelewa husababisha ulemavu na matatizo makubwa
Pia mkurugenzi wa CHT, Bwana Hakim alitoa maoni: "Ninawahimiza viongozi wa mashirika ya wazazi kuelimisha na kuhamasisha wazazi kuhusu jukumu lao la kuhakikisha matibabu ya mapema kwa watoto wao, hata mbele ya changamoto za kifedha. Wakati wahisani wanapatikana kusaidia juhudi hii, nao pia wana mipaka. Kama mzazi wa mtoto aliye na ulemavu, naelewa changamoto zinazokuja na kutoa huduma muhimu. Hata hivyo, ninawahimiza wazazi wenzangu kufanya juhudi kuharakisha watoto wao kwenda kwenye vituo vya afya vinavyotumika kusaidia watoto, ili kuzuia matatizo yanayojitokeza kutokana na matibabu ya kuchelewa." anasema Mkurugenzi wa CHT.
*Video Credit: Taasisi ya Orthopaedic ya Muhimbili (MOI)
Tafsiri/Manukuu: CHT
swSwahili